NGUVU YA IBADA KATIKA KULINDA SIHA
NJEMA
Hivi karibuni Mamlaka za Afya za karibu nchi zote duniani zimeibuka na miongozo miwili mipya kuhusu unyonyeshaji wa ziwa la mama kwa watoto wachanga. Muongozo wa kwanza ni ule unaoongeza muda wa mtoto mchanga kuweza kuishi kwa ziwa la mama yake pekee bila kuhitaji msaada wa chakula kingine, kutoka miezi mitatu hadi miezi sita.
Muongozo wa pili ni ule unaotoa ruksa kwa kina mama walioathiriwa na virusi vya ukimwi, na hasa katika nchi zinazoendelea, kunyonyesha watoto wao kama kawaida, alimradi tu wazingatie maelekezo ya wataalamu wa afya.
Kuibuliwa kwa miongozo hii ni matokeo ya tafiti mpya za hivi karibuni kabisa kuhusu nafasi ya ziwa la mama katika siha ya mwanadamu. Kwa mujibu wa tafiti hizi miongoni mwa faida zinazopatikana kwa kumnyonyesha mtoto ziwa la mama yake pekee kwa muda usiopungua miezi sita ni pamoja na:
1. Mtoto husika hupungukiwa na uwezekano wa kupata maambukizi hatari kwenye masikio, kwenye

utumbo, na kwenye njia ya hewa;
2. Kwa maisha yake yote mtoto husika hupungukiwa na uwezekano wa kupata pumu na magonjwa mengine

ya mzio (allergies);
3. Kwa maisha yake yote mtoto husika hupungukiwa na uwezekano wa kupata kisukari (cha utotoni na

ukubwani);
4. Kwa maisha yake yote mtoto husika hupungukiwa na uwezekano wa kupata ugonjwa wa Celiac (Celiac

disease) – yaani uharibifu wa
utando wa ndani kwenye utumbo mwembamba kunakotokana na
kushambuliwa na kinga
za mwili pale mhusika anapotumia kiini lishe cha ‘gluten’, kinachopatikana
kwenye
nafaka, hususan ngano;
5. Kwa maisha yake yote mtoto husika hupungukiwa na uwezekano wa kupata mfuro (inflammation)

kwenye utumbo mpana na
mkunduni, hali inayojulikana zaidi kama ‘Ulcerative colitis’;
6. Kwa maisha yake yote mtoto husika hupungukiwa na uwezekano wa kupata uvimbe mwako kwenye

sehemu ya mwisho ya utumbo mwembamba na
sehemu ya kwanza ya utumbo mpana, hali inayojulikana
zaidi kama Crohn’s
disease;
7. Mama anayehusika hupungukiwa na uwezekano wa kuvuja damu nyingi kupindukia wakati anapojifungua

kwa njia ya kawaida
(postpartum hemorrhage); na
8. Mama anayehusika hupungukiwa uwezekano wa kupata saratani za matiti na mfumo wa uzazi.
Aidha tafiti zinaonyesha kuwa kadri mtoto anavyoongezewa muda wa kunyonya (zaidi ya miezi 6) ndivyo anavyozidi kuimarika kiakili, kimwili na kisaikolojia. Kutokana na tafiti hizi Shirika la Afya Duniani (WHO) limekuwa likisisitiza umuhimu wa kina mama kuwanyonyesha watoto wao kwa muda wa miaka miwili au zaidi. Zifuatazo ni nukuu za Wataalamu kadhaa wakiunga mkono mtizamo huu:
“Tumekuwa tukiona kuwa watoto walioachishwa kunyonya mapema wanaonyesha dalili zote za magonjwa yanayooanishwa na kuacha kunyonya mapema: uchokozi, hasira kali, tabia inayoonyesha kupagawa, ung’ang’anizi kwa wanaowahudumia na uwezo mdogo wa kujenga mahusiano ya kina. Unyonyeshaji unaonyesha kudhibiti tabia za kikorofi kwa watoto walioanza kutembea (toddlers) na kuweka uwiano mzuri katika tabia zao”– Dr William Sears, The Discipline Book, 1997
“…, Siku zote nimekuwa nikitoa changamoto kwa mfumo wetu wa kudhibiti uhalifu (the criminal justice system) kunionyesha muuaji mmoja, mbakaji mmoja, or teja mmoja (drug addict) katika gereza lolote la America ambaye alinyonyeshwa ziwa na mama yake kwa miaka miwili au zaidi, kama ilivyopendekezwa na Shirika la Afya Duaniani” – Dr James Prescott, ‘Touch the Future’, Spring 1997.
“ Katika karne hii, muda unaochukuliwa kuwa ni sawa kuwaachisha watoto ziwa umepungua hadi kufikia miazi mitatu. Kwa ujumla jamii imekuwa haijali mahitaji halisi ya watoto. Hata hivyo katika maeneo mbalimbali ya dunia maamuzi ya kumuachisha mtoto ziwa yanaachwa kwa mtoto mwenyewe. Hii ndiyo sawa, watoto wanatakiwa wajiachishe wenyewe kunyonya. Kwa wale wanaopewa fursa hiyo kwa kawaida hujiachisha wakiwa na umri wa wastani wa miaka 4.2. Katika kitabu chake, Breastfeeding: A Guide for the Medical Profession, Daktari Ruth A. Lawrence, M.D. anasema kuwa unyonyeshaji unaolenga burudani zaidi kuliko lishe ni muhimu kwa watoto wenye umri unaozidi miaka miwili.”
….
“Kupakatwa na kunyonyesha ni tabia zinazojenga mahusiano ya kina katika miaka ya mwanzo ya maisha ya mtoto. Unyonyeshaji wa kilishe na ule wa burudani ni muhimu kwa watoto wa mwaka mmoja, miwili, mitatu, na minne” – Peter Ernest Haiman, PhD, Berkeley CA, U.S.A., New Beginnings, Jan/Feb 1994
Mambo haya yanaweza kuonekana mageni kwa mwananchi wa kawaida (asiye mtaalamu wa masuala ya unyonyeshaji) na ambaye si mfanya ibada. Hata hivyo kwa watu wa ibada haya ni mambo ambayo wamekuwa wakiyafanya kama wajibu kwa zaidi ya miaka 1,400.
Je, kuna ushahidi wowote wa hili?
Quran tukufu (2:233) inaelekeza:
“ Na wanawake waliozaa wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili, kwa anayetaka kukamilisha kunyonyesha; na ni juu ya baba ya (yake) chakula chao (hao watoto na mama) na nguo zao kwa sharia. Wala haikalifishwi nafsi yoyote ila kwa kadri ya wasaa wake. Mama asitiwe taabuni kwa ajili ya mtoto wake, wala (baba) asitiwe taabuni kwa ajili ya mtoto wake. Na kama wote wawili wakitaka kumwachisha ziwa (kabla ya miaka miwili), kwa kuridhiana na kushauriana basi si kosa juu yao. Na kama mkitaka kuwapatia watoto wenu mama wa kunyonyesha (wengine wasiokuwa mama zao), basi haitakuwa dhambi juu yenu kama mkitoa (kuwapa hao wanyonyeshaji) mlichowaahidi kwa shariah. Na mcheni Mwenyezi Mungu na jueni kwamba Mwenyezi Mungu anayaona yote mnayoyatenda.”

No comments:
Post a Comment