Wednesday, June 8, 2016

NGUVU YA IBADA KATIKA KULINDA SIHA NJEMA: CONNECTION YA MAVAZI


NGUVU YA IBADA KATIKA KULINDA SIHA NJEMA

Uvaaji ni moja ya ibada muhimu sana. Kwa baadhi ya imani, kwa mfano Uislamu, kuna ibada nyingi muhimu ambazo kukubalika kwake kunategemea kwanza usahihi wa ibada hii ya uvaaji. Kwa mfano, vazi la mwanamume wa kiislamu kwa kiwango cha chini kabisa ni lazima liwe ni lile linalofunika kati ya kitovu na magoti. Aidha, vazi la mwanamke wa kiislamu ni lazima liwe ni lenye kumfunika mwili wote isipokuwa uso, viganja vya mikono, na nyayo. Aidha kwa mwanamke ni lazima vazi hilo lisimbane na kuonyesha ramani ya maumbile yake.

Swala/Sala kwa Muislamu ni ibada kubwa sana kwa kuwa pia ni miongoni mwa nguzo tano za dini hiyo. Sasa tazama umuhimu wa ibada ya uvaaji kwa kipimo cha swala ya kiislamu. Muislamu wa kiume au wa kike anaweza akaswali swala kwa umakini na kwa kuzingatia taratibu zake zote, lakini kama atakuwa hakutimiza masharti ya ibada ya uvaaji kwa mujibu wa maelezo hayo hapo juu, atakuwa hana swala! Sina hakika sana lakini nadhani hata maandiko ya dini nyingine yana maelekezo yanayofanana na hayo.

Baada ya kujenga hoja hii inayoonyesha kwamba uvaaji ni moja ya ibada muhimu kabisa sasa tunatakiwa tujiulize: Je, kuna uhusiano wowote kati ya mavazi na afya? Jibu ni ndiyo. Ni ndiyo kwa sababu uvaaji una uhusiano mkubwa sana na mfumo wa kuondoa taka mwilini (lymphatic system). Mfumo huu unajumuisha chembechembe nyeupe za damu ambazo kazi yake ni ya uaskari wa mstari wa mbele kwenye kupambana na uvamizi wowote mwilini, majimaji yasiyo na rangi yaitwayo lymph ambayo kazi yake ni kusafirisha chembe hizo nyeupe za damu pamoja na kuondoa sumu na mabaki mengine yasiyofaa kutoka mwilini hadi katika maeneo ya kutolea nje, na mtandao wa mirija ambayo hupitisha maji hayo (lymph) ambayo huishia kwenye vinundu (nodes) vyenye kazi ya kuchuja maji hayo, kabla ya kurudishwa mwilini kuendelea na kazi yake. Kwa kuwa robo tatu ya mirija tuliyoitaja iko juu juu karibu sana na ngozi, ina maana kuwa ngozi inapobanwa, na sehemu kubwa ya mirija hii nayo hubanwa pia.

Ubanifu huu hufifisha uwezo wa mirija hii kufanya kazi na mwisho wa siku mvaaji huathirika kiafya. Hii ina maana kuwa nguo za kubana, viatu vya kubana na hata mikanda ya kubana sana ni vitu vya kuepukwa. Kwa mfano, imebainika kuwa uvaaji wa sidiria zinazobana ni moja ya vyanzo vikubwa vya saratani ya matiti!
Dr. Michael Schacter, katika makala yake ‘The Prevention and Complementary Treatment of Breast Cancer’ anaandika.

“Over 85% of the lymph fluid flowing from the breast drains to the armpit lymph nodes. Most of the reast drains to the nodes along the breast bone. Bras and other external tight clothing can impede flow. The nature of the bra, the tightness, and the length of time worn, will all influence the degree of blockage of lymphatic drainage. Thus, wearing a bra might contribute to the development of breast cancer as a result of cutting off lymphatic drainage, so that toxic chemicals are trapped in the breast” .

Maana ya maelezo haya ya Dr Schacter kwa tafsiri ya kiswahili isiyo rasmi ni:
“Zaidi ya 85% ya lymph inayosafisha titi husafiri na huchuruzikia kwenye vinundu (nodes) vilivyoko kwapani. Lymph iliyobaki husafiri na kuishia kwenye vinundu vilivyoko kwenye mfupa wa titi. Sidiria na mavazi mengine ya nje yanayobana yanaweza kupunguza ufanisi wa mchuruziko huu wa lymph. Aina ya sidiria, kiasi inachobana, na urefu wa muda wa kuivaa vyote kwa pamoja vitaamua kiasi cha punguzo la ufanisi wa huu mchuruziko. Kwa maana hii uvaaji wa sidiria unaweza kuchangia kuibuka kwa saratani ya matiti, kutokana na uzuiaji wa mchuruziko wa lymph, kitu ambacho kinapelekea chemikali za sumu kubaki ndani ya titi’

Aidha kwa mujibu wa Dr. David Agus, mwandishi wa kitabu cha ‘End of Illness’, mavazi ya kubana huathiri sehemu zote zinazobanwa kwa njia nyingine zaidi ya ile ya kuathirika kwa mfumo wa lymph. Dr. Agus anasema kuwa sehemu zote zinazobanwa zinazaa uvimbe mwako (inflammation), na uvimbe mwako ni chanzo kikubwa sana cha maradhi mengi ya kimfumo.
Tunapaswa tujiulize. Hivi inalipa kweli kuvaa mavazi kwa dhana ya kwamba tunafurahisha watu wengine (watatusifu!) na huku tukiweka jiwe la msingi la maradhi ambayo yanaweza yakagharimu maisha yetu?




No comments:

Post a Comment