Mfuro ni kitu gani?
Umeshawahi kujikwaa ukiwa hukuvaa viatu? Au
umeshawahi kujigonga/kugongwa kwa nguvu kidogo, hasa kichwani au kwenywe paji
la uso? Inawezekana baada ya matukio haya ulishuhudia uvimbe katika vidole vya
mguu, au nundu katika kichwa au paji lako la uso. Basi huo ni mfuro.
Ukiachilia mbali mifuro inayosababishwa na kujiumiza
kimwili moja kwa moja kama tulivyoeleza katika hiyo mifano hapo juu, seli zetu
za mwili kuanzia za ndani hadi zile za nje huweza kupatwa na mfuro kwa sababu
nyingine mbalimbali.
Kwa kawaida kinga za mwili zinapoingia kupambana na
kitu chochote kile zinachikidhania ni hatari kwa mwili, moja ya matokeo katika
eneo la mapambano ni mfuro. Hii ina maana kwamba kila unapopata maambukizi
yoyote yale, pamoja na ugonjwa wenyewe unaosababishwa na hayo maambukizi,
sehemu ya maamivu unayokabiliana nayo hutokana na kuenea kwa mfuro mwilini.
Kwa bahati mbaya sana maisha ya kisasa yametawaliwa
na vitu vingi sana vinavyosababisha kinga za mwili ziwe katika mkao wa vita
muda wote. Vitu hivi ni pamoja na baadhi
ya vyakula; vinywaji ; dawa (hususan zile za kifamasia); na vipodozi. Baadhi ya
vitu hivi vinapoingia ndani ya mwili huchochea kinga za mwili kudhani kuwa adui
kaingia; na kwa hivyo moja kwa moja huingia katika mapambano. Kwa kuwa vitu
hivi tunakutana navyo kila siku na kila mara, hii ina maana kuwa miili yetu
inakabiliwa na mfuro karibu muda wote. Inaaminika kuwa miongoni mwa vyakula vinavyochochea
mfuro kwa kiwango cha juu sana ni nafaka zote zilizochakatwa (kuondoa ganda la
juu); sukari; na mafuta yanayotokana na mbegu pale yanapotumiwa kwa matumizi ya
kupikia. Mafuta ya mbegu ni pamoja na
yale ya alizeti, ufuta, mawese, karanga, pamba, nakadhalika.
Kitu kingine kinachosababisha mfuro endelevu ni
mtindo wa maisha wa kubweteka. Kiasili hatukuumbwa tuwe ni watu wa kutulia eneo
moja kwa muda mrefu. Maumbile yetu
yanahitaji viungo vyetu viwe vinajongea muda mwingi pale tunapokuwa tuko macho.
Tafiti zimebainisha kuwa kuketi au kujilaza sehemu moja muda mrefu (nusu saa au
zaidi) kunauingiza mwili uwe katika hali ambayo inasababisha mfuro katika seli.
Moja ya namna za kutambua kiwango cha mfuro mwilini ni kupima kiwango cha
chembechembe zinazoitwa C- Reactive Protine (CRP). Tafiti zinaonyesha kuwa CRP
inaongezeka katika mzunguko wa damu kwa kitendo cha kuketi tu sehemu moja kwa
muda mrefu.
Madhara ya Mfuro.
Umeshawahi kukutana na tukio la kusumbuliwa na
mlango wa mbao wakati wa kuufunga au kuufungua, hususan wakati wa msimu wa
mvua? Kuna baadhi ya mbao zina tabia ya kunyonya unyevu unyevu na kufura.
Milango au madirisha yanayotengenezwa na aina hii ya mbao mara nyingi inaweza
ikasumbua wakati wa kufunga au kufungua
wakati wa vipindi vya mvua endelevu.
Mfano huu ni sawa na kinachotokea kwenye seli inayokabiliwa na mfuro.
Kila seli ina vitu vinavyoitwa ‘vipokezi’ au kwa
kitaalamu cell receiptors. Vipokezi hivi ni sawa na milango na madirisha. Moja
ya kazi ya vipokezi hivi ni kupokea viini-lishe, maji na gesi ya oxygen kutoka
nje ya seli na kuviingiza ndani ya seli kwa ajili ya majukumu mbalimbali. Kazi nyingine ni kutoa nje ya seli uchafu wa
mabaki ya viini-lishe, maji yaliyotumika na hewa chafu kwa ajili ya kuondolewa
mwilini.
Vipokezi kwenye seli yenye mfuro ni sawa na mbao ya
dirisha au mlango inayonyonya unyevu nyevu. Mfuro hupelekea vipokezi hivi visifanye kazi
kwa ufanisi. Wataalamu wengi wanaamini kuwa kutokana na hali ya miili yetu
kukabiliwa na mfuro ambao ni endelevu, ufanisi wa vipokezi katika seli zetu uko
chini sana na hali hii ndiyo chimbuko kubwa la maradhi mengi ya kimfumo, ikiwa
ni pamoja na ugonjwa wa kisukari.
Chukua Hatua Kukabiliana na Mfuro
Hatua muhimu katika kukabiliana na mfuro ni pamoja
na:
- Kuacha kula
vyakula vinavyochochea mfuro. Kama ambavyo tumekwishaona, vyakula hivi ni
vile vyote vinavyotokana na nafaka
zilizochakatwa. Vingine ni SUKARI na vile vilivyopikwa kwa mafuta ya
mbegu, yaani vegetable oils;
- Kuvifanya
viungo vyote vya mwili viwe katika hali ya kujongea (move) kila mara. Ni
vema kutoruhusu kuketi sehemu moja kwa muda unaozidi nusu saa. Nyanyuka,
jinyooshe, tembea hatua mbili tatu, kisha rejea kwenye kiti chako kila
baada ya muda fulani. Mazoezi ya viungo ya walau siku nne kwa wiki ni
msaada mkubwa. Hata hivyo pale ambapo fursa ya kufanya mazoezi ni finyu,
ni muhimu kutenga muda kila siku na kutembea kwa mguu kiasi cha kiliometa
tatu au nne;
- Hakikisha unajitibu
magonjwa yote ya maambukizi yaliyoko mwilini mwako; na
- Jenga tabia ya kula au kunywa vitu vyenye sifa ya kukabiliana na mfuro. Baadhi ya vitu hivi ni pamoja na:
- Viungo
kama manjano; tangawizi; karafuu; jira (binzari nyembamba); na habat
Sauda (black seed);
- Chai ya
kijani (green tea); na
- Matunda kama zabibu, zambarau






No comments:
Post a Comment