Wednesday, June 8, 2016

UNAJUA NI KWA NINI WAINGEREZA WAMEITWA LIMEY?


Kwenye karne ya 18 kurudi nyuma mabaharia wengi sana (hasa wale wa vyombo vya kijeshi) waliangamia kutokana na ugonjwa wa kiseyeye (scurvy). Huu ni ugonjwa ambao unashambulia tishu za mwili zinazotumika kama viungio au daraja (connective tissue) baina ya viungo mbalimbali ndani ya mwili.

Awali haikujulikana ni kitu gani kilikuwa kinasababisha ugonjwa huu. Kwenye karne ya 18 daktari mmoja wa Kiingereza mwenye asili ya Scotland aliyejulikana kama James Lind alishauri kuwa mabaharia wachanganyiwe juisi ya ndimu ama limao kwenye vinywaji vyao. 

Ushauri huu ulizaa matokeo mazuri kwani ugonjwa wa kiseyeye ulitoweka miongoni mwa mabaharia wa Kiingereza. Kufuatia hali hii jeshi la wanamaji la Ungereza liliweka sera kuwa ni lazima meli zote za kijeshi za jeshi hilo ziwe na kiasi cha kutosha cha juisi ya ndimi au limau. Kufuatia hali hii watu wa mataifa mengine walianza kuwatania Waingereza kwa kuwapachika jina la 'limey', au 'Walami'- kama ambavyo Waswahili tumekuwa tukiwaita -  kuonyesha mahusiano yao na limau. Limau kwa kiingereza huitwa 'lime.'  

  

No comments:

Post a Comment