Bambia ni mboga ambayo watu wengi huidharau sana! Kwa sababu ya dharau hii wateja wake ni wachache, na kwa maana hiyo basi imelundikana huko masokoni kwa bei ya kutupa!
Wangejua tu!
Hali iko hivyo kwa sababu watu wengi hawajui faida za kiafya za kula bamia. Miongoni mwa faida hizi ni pamoja na:
1. Kuzuia uyabisi wa tumbo. Kama una matatizo ya kupata choo haraka sana anza kutumia bamia!
1. Kuzuia uyabisi wa tumbo. Kama una matatizo ya kupata choo haraka sana anza kutumia bamia!
2. Huimarisha sana uwezo wa macho kuona. Tafuna bamia ndugu yangu kama unaona macho kidogo yana mtihani!
3. Kina mama wajawazito bugia sana mlenda! Mlenda ni moja ya vyakula vitakavyomsaidia huyo mwanao huko tumboni kukua vizuri sana kutokana na wingi wa vitamin ya folate iliyomo.
4. Bamia huimarisha sana chembechembe nyeupe za damu na kwa maana hiyo huboresha kinga za mwili.
5. Kama una maumivu maumivu ya mifupa unaweza kunufaika kwa kula bamia. Bamia ina kiwango kikubwa cha vitamin K. Hii ni moja ya vitamini zinazohitajika kuyawezesha madini ya kalisi (calcium) kubaki kwenye mifupa!
6. Damu yako ina matatizo ya kuganda? Bamia ni jibu. Kutokana na kuwepo kiasi kikubwa cha vitamin K, basi damu yako itakuwa kwenye mazingira mazuri ya kuganda pale itakapohitajika.
7.Kisukari! Wewe ni mgonjwa wa kisukari? Basi ifanye bamia kuwa mmoja wa marafiki zako wakubwa kabisa!
8. Saratani? Hivi karibuni imevumbuliwa kuwa bamia ina viambata ambavyo vina uwezo wa kupambana na kuua seli za saratani.
Gonga mlenda! ENJOY







No comments:
Post a Comment