BIDHAA ZETU


JINA LA BIDHAA MARADHI NA MATUMIZI
HAIIBA TIMAMU TEA
Tangu kuingia sokoni kwa Chai ya Haiiba Timamu, baadhi ya watu wamekuwa wakiuliza iwapo wanaweza kuitumia hata kama hawana tatizo lolote la kiafya. Ili kupunguza wingi wa wanaouliza swali hili ni vema tukafikisha kwa wasomaji makala kadhaa fupi zinaZolenga kujibu swali hili. Kila makala itajikita katika kuzungumzia manufaa na faida za kiafya za kila moja, kati ya makundi mbalimbali ya viini lishe yaliyomo kwenye hii Chai ya Haiiba Timamu. Makala ya leo itazungumzia kundi la vitamini. Hata hivyo, kama utangulizi, kwa minajili ya kueleweka zaidi, ni vema wasomaji wetu wakatambua kuwa magonjwa yamegawanyika katika makundi mawili makuu

MARADHI YA KUAMBUKIZA

Kundi la kwanza ni lile la maradhi ya kuambukiza. Haya ni,yale maradhi yanayozaliwa mwilini kutokana na mwili kuvamiwa na vimelea hai,vyenye uwezo wa kusababisha maradhi pale ambapo vimelea husika vitakuta kinga za mwili za,mhusika zinafanya kazi chini ya kiwango. Vimelea hivi ni bacteria, virusi,,fangasi, protozoa, minyoo na aina ya chembechembe za protini zinazoitwa prions. Mfano wa magonjwa yanayosababishwa na vimelea hivi ni kama malaria,,kipindupindu, kifua kikuu, nakadhalika. Aghalabu tiba ya maradhi haya huwa ni,kutumia dawa ikiwa katika dozi maalum kwa njia ya kunywa, sindano au dripu, na wakati mwingine kwa,kupaka. Kwa kifupi mgonjwa mwenye uzito fulani, anatakiwa atumie dawa fulani, yenye nguvu fulani, kwa mpangilio fulani kwa kutwa, na kwa,idadi ya siku fulani.

MARADHI YA KIMFUMO
Kundi la pili ni lile la maradhi ya kimfumo (metabolic,diseases). Haya ni yale magonjwa yanayozaliwa mwilini kutokana na mifumo ya mwili kushindwa kufanya kazi kwa utaratibu uliokusudiwa. Kwa mfano, kiasi cha,sukari kwenye damu ya mtu wa kawaida (siyo mgonjwa wa kisukari) kinatakiwa kiwe chini ya 7.7 mmol/l (140 mg/dl), kiasi cha masaa mawili hivi baada ya,kula. Kiasi hiki kikiwa juu ya hapa maana yake ni kwamba mfumo wa mhusika wa,kuhamisha sukari kutoka kwenye damu na kuipeleka huko kwenye seli inakotakiwa iwepo haufanyi kazi inavyotakiwa.

Mfano mwingine. Mtu ambaye siyo mgonjwa anatakiwa kuwa na kiwango cha juu cha shinikizo la damu cha kati ya mmHg,110 – 120; na kiwango cha chini cha mmHg 80. Nje ya viwango hivi maana yake,ni kwamba kuna shida katika eneo fulani la mfumo wa mzunguko wake wa damu. Shida inaweza kuwa mishipa ya damu imekakamaa na hainyumbuliki kupanuka pale,inapohitajika, na kwa maana hiyo shinikizo la damu linakuwa kubwa kwenye kuta za mishipa hiyo pale damu inaposukumwa kusambazwa mwilini. Shida pia inaweza kuwa kasi ndogo ya utaratibu wa uvunjifu na uundaji wa kemikali mwilini (slow metabolism), hali inayopelekea kasi ndogo ya usukumaji wa damu wakati wa,kuisambaza mwilini na hivyo kuweka shinikizo dogo katika kuwa za mishipa ya damu.

Aghalabu maradhi ya kimfumo yanasababishwa na mambo manne makuu ambayo ni:

1. UPUNGUFU WA VIINI LISHE
Upungufu wa viini lishe na virutubisho fulani fulani ndani ya mwili. Kwa mfano maji; madini lishe, vitamini, tindikali mafuta zisizozalishwa mwilini (essential fatty acids), vizuia,vioksidishaji (anti-oxidants), na vijenzi vya protini visivyozalishwa mwilini,(essential amino acids).

2. VYAKULA VISIVYOFAA
Ulaji wa vyakula,visivyokubaliwa na mwili, kwa mfano sukari ya viwandani na baadhi ya vyakula,vingine, haswa vile vilivyochakatwa (processed).

3.MLUNDIKANO WA SUMU MWILINI
Sumu mbalimbali zinazolundikana mwilini kupitia taka zinazobaki mwilini baada ya mchakato wa kutoa nishati na viini lishe kutoka katika chakula tunachokula, na sumu mbalimbali zilizoingia mwilini kwa njia ya chakula, vinywaji, dawa, vipodozi na hewa chafu. Mifano ya sumu hizi ni:

(a) Jivu la tindikali linalobaki baada ya vyakula vya protini na wanga tunavyokula kuchakatwa ndani ya mwili.

(b) Kemikali mbalimbali zinazoingizwa,mwilini kutokana na vinogesho (sweeteners) mbalimbali bandia vinavyotumika kwenye vinywaji mbalimbali hasa vile vinavyotangazwa kuwa havitiwi sukari.

(c) Kemikali mbalimbali zinazoingizwa mwilini kutokana na kemikali mbalimbali zinazotumiwa kwenye vyakula na vinywaji kama vihifadhi (chemical preservatives), na viongeza ladha (flavor enhancers).

(d) Kemikali mbalimbali zinazoingizwa,mwilini kutokana na kutumia maji,‘yaliyotakaswa’ na kemikali kama chlorine na Aluminum sulfate.

(e) Mvuke wa zebaki (mercury) unaoingia mwilini kutokana na mchanganyiko wa kuzibia matundu ya meno unaohusisha madini ya fedha na zebaki (mercury amalgam).

(f) Nakadhalika.

4. MSONGO
Msongo endelevu (chronic stress). Msongo endelevu ni tishio kubwa sana kiafya. Sababu kubwa ni kwamba mwili huzalisha tindikali nyingi sana pale mtu anapokabiliwa na,msongo. Hii ni kutokana na ukweli kwamba msongo endelevu hutumia nishati nyingi sana ya mwili na matumizi,yoyote ya nishati huzaa tindikali kama zao la ziada (by product).

Aidha, homoni mbalimbali zinazozalishwa na mwili ili kukusaidia kukabiliana na,msongo zina kawaida ya kuharibu vinasaba vya seli (DNA) iwapo zitaachwa mwilini,kwa muda mrefu bila kuondolewa. Uharibifu wa vinasaba huzaa maradhi mengi sana ndani ya mwili, na haswa saratani. Mfano wa maradhi ya kundi hili la maradhi ya kimfumo ni kisukari, ugonjwa wa ini bonge (fatty liver disease), shinikizo la damu (hypertension), ugonjwa wa moyo, ugonjwa wa jongo, saratani, magonjwa ya mifupa, magonjwa ya misuli, nakadhalika. Ili kujihakikishia uhuru,wa kuishi bila kukumbwa na maradhi haya ni muhimu kuishi maisha ambayo kwa kiasi kikubwa yatakuwa yamejiweka mbali na visababishi hivi.

1

Baada ya utangulizi huu sasa ni wakati muafaka,wa kuingia katika sehemu ya kwanza ya maelezo juu ya Haiiba Timamu Tea, ambayo kama tulivyotangulia kuitambulisha,hapo awali, inahusu kundi la viini lishe vilivyomo ndani yake vinavyojulikana kama vitamini. Huu utakuwa ni mwanzo wa majibu ya swali tuliloulizwa,kuhusiana na ni nani anapaswa kutumia Timamu Tea.
HAIIBA TIMAMU TEA
VITAMINI NI NINI?

Vitamini ni kemikali ya kiorganiki,(moja ya viasili vyake ni carbon) ambayo mwili unaihitaji kwa ajili ya kuendeleza uhai, lakini mwili hauna uwezo wa kuizalisha kwa kiwango cha kutosha, au hauna uwezo wa kuizalisha kabisa. Upungufu wa vitamini hupelekea kuathirika kwa ile michakato ya kibailojia inayosukumwa na vitamini hiyo na hivyo kusababisha mapungufu katika hiyo michakato.  Mapungufu husika kuzaa ugonjwa au magonjwa yanayohusiana na upungufu huo.

Kwa kawaida huwa tunatakiwa tupate vitamini zote tunazohitaji kupitia katika lishe. Hata hivyo kutokana na mapungufu,mbalimbali yaliyoko katika lishe zetu inatokea tukawa na upungufu wa baadhi ya vitamini na hivyo kukumbwa na magonjwa yanayohusiana na huo upungufu.

VITAMINI MUHIMU ZILIZOMO KATIKA HAIIBA TIMAMU TEA.

Baadhi ya vitamini muhimu zilizomo kwa wingi katika Chai ya Haiiba Timamu ni B1, B2, B3 na C.

Vitamini B1

Faida za Vitamini B1 ni nyingi. Faida tano muhimu nipamoja na:

  1.  UZALISHAJI WA NISHATI MWILINI
    Vitamini hii ina jukumu la kusaidia kubadilisha sukari kuwa nishati. Katika kutimiza jukumu hili inafanya kazi kama kimeng’enya kinachooksidisha sukari (kuiongezea gesi ya oksigeni) ili kuibadili kuwa nishati kwa ajili ya kuendesha vyema shughuli mbali mbali za viungo nyeti vya mwili kama ubongo, moyo, mapafu na figo.

  2. UTENDAJI KAZI WA MFUMO WA MZUNGUKO WA DAMU
    Vitamini hii inajukumu la kuzalisha kemikali tarishi (neurotransmitter) inayoitwa,acetylcholine. Kazi ya kemikali tarishi hii ni kupeleka taarifa mbalimbali baina ya misuli na mishipa ya fahamu. Upungufu wa kemikali hii hupelekea mapigo ya moyo kutokuwa katika mpangilio unaoeleweka (irregular heart-beat). Upungufu mkubwa unaweza kupelekea kwenye moyo kushindwa kufanya kazi.

  3. KUKINGA MACHO DHIDI YA UGONJWA WA MTOTO WA JICHO (CATARACT)
    Vitamini B1 kwa pamoja na tindikali za muhimu za mafuta za omega 3 na omega 6 huzuia ugonjwa wa macho unaohusiana na lenzi za macho kutanda ukungu ambao ni maarufu wa jina la mtoto wa macho.

  4.  KUSAIDIA UBONGO KUFANYA KAZI VIZURI
    Vitamini hii husaidia kuboresha utunzaji wa kumbukumbu na umakini, huimarisha mishipa ya fahamu na hukinga dhidi ya magonjwa mbalimbali yanayohusisha kudhoofika kwa ubongo.

  5.  KUIMARISHA MISHIPA YA FAHAMU
    Husaidia kuimarika na kuboreka kwa utando unaozunguka mishipa ya fahamu na hivyo kutoa kinga dhidi ya uchakavu wa mishipa hiyo.
Vitamini B2
Faida za Vitamini B2 ni nyingi. Faida tano muhimu ni,pamoja na:
  1. MAUMIVU
    Huzuia maumivu makali ya kichwa yanayoambatana na dalili nyingine kama kichefuchefu,,kutapika, kushindwa kuhimili mwanga mkali na kelele, na wakati mwingine kuona vimulimuli na kuhisi kama kuna kuchomwa chomwa na sindano kwenye mikono na miguu.

  2. KIZUIA KIOKSIDISHAJI
    Hufanya kazi kama kizuia kioksidishaji kinachosaidia kukinga dhidi ya magonjwa ya moyo na saratani.
  3. UPUNGUFU WA DAMU NA UGONJWA WA SELI MUNDU
    Husaidia katika kutibu maradhi ya upungufu wa damu na seli mundu (sickle cell).
  4. KINGA DHIDI YA VICHOCHEO VYA SARATANI
    Husaidia kupambana na vitu vinavyochochea saratani mwilini (carcinogens)
  5. UCHAKATAJI WA PROTINI, WANGA NA MAFUTA MWILINI
    Husaidia katika uchakataji wa protini, mafuta na wanga na hivyo katika uzalishaji wa nishati mwilini.
Vitamini B3
Faida za Vitamini B3 ni nyingi. Faida nne muhimu ni pamoja na:
  1. UGONJWA WA MOYO
    Husaidia sana katika kuulinda mwili wako dhidi ya ugonjwa wa moyo.
  2. LEHEMU (CHOLESTEROL)
    Husaidia kupunguza kiwango cha lehemu mbaya (bad cholesterol) mwilini na kuongeza kiasi cha lehemu nzuri (good cholesterol) mwilini.
  3. KUPOTEZA KUMBUKUMBU NA MAGONJWA MENGINE
    Tafiti pia zinaonyesha kuwa vitamini hii husaidia sana kupambana na ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu; ugonjwa wa lenzi za macho kufunikwa na ukungu,(cataracts); ugonjwa wa mifupa dhaifu; na ugonjwa wa kisukari cha udogoni (Type I diabetes).
  4. UZALISHAJI WA NISHATI NDANI YA SELI ZA MWILI NAKADHALIKA
    Aidha, vitamini hii imehusishwa na kusaidia kuboresha uzalishaji wa nishati katika ngazi ya seli; kuboresha na kuimarisha mishipa ya fahamu; na kuimarisha na kuboresha mfumo wa usagaji wa chakula.
     
Vitamini C
Hii ni vitamini yenye faida nyingi sana muhimu kiafya. Baadhi ya faida hizi ni pamoja na:
  1. UGONJWA WA MAFUA
    Husaidia kupunguza ukali wa ugonjwa wa mafua na muda wa kuugua ugonjwa huo.
  2. MIZIO
    Huzuia mizio (allergies) kwa kusaidia kudhibiti uwepo wa homoni ya Histamine ndani ya mwili.
  3. MAGONJWA YA NGOZI
    Ni tiba ya asili ya magonjwa ya ngozi ikiwa ni pamoja na kupunguza kasi ya kuzeeka kwa ngozi na kutengeneza makunyanzi.
  4. MAJERAHA
    Inasaidia sana katika kutibu majeraha.
  5. ATHARI ZA MSONGO
    Inazuia athari za msongo katika mwili.
  6. INASAIDIA KATIKA UTENGENEZAJI WA COLLAGEN
    Inawezesha ujenzi wa protini muhimu ya collagen ambayo ni muhimu katika tishu zinazofanya majukumu ya kuunganisha viungo mbalimbali vya mwili (connective tissue). Kiwango kidogo cha uundwaji wa collagen kunaweza kusababisha ugonjwa hatari wa scurvy.
  7. LEHEMU (CHOLESTEROL)
    Inasaidia kupunguza kiwango cha lehemu (cholesterol) katika mzunguko wa damu
  8. UNYUMBUFU WA MISHIPA YA DAMU
    Inasaidia kudumisha unyumbufu wa mishipa ya damu (elasticity) na hivyo kupunguza uwezekano wa kupata shinikizo la damu na maradhi ya moyo
  9. KIZUIA KIOKSIDSHAJI CHENYE NGUVU
    Husaidia sana kuzimua chembechembe zenye umeme chanya mwilini (free radicals) na hivyo kuzuia chembe hizo kufanya,uharibifu katika mfumo wa mzunguko wa damu mwilini na kusababisha magonjwa ya,moyo na kiharusi
  10. URATIBU WA SUKARI KWENYE DAMU
    Inasaidia,katika uratibu wa sukari kwenye damu na kupunguza madhara yanayosababishwa na,kiwango kingi cha sukari kwenye damu
  11. MATIBABU YA SARATANI
    Inasaidia katika matibabu ya saratani. Tafiti zinaonyesha kwamba dozi kubwa za vitamini,C ni mujarabu sana katika maangamizi ya seli za saratani
  12. KUPOTEZA KUMBUKUMBU
    Ongezeko la vitamini C mwilini husaidia sana kudhibiti mwendelezo wa ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu pamoja na magonjwa mengine yanayoathiri mishipa ya,fahamu
  13. UPANA WA NJIA YA HEWA
    Husaidia sana kuzuia kupungua kwa upana wa njia ya hewa kunakoweza kuleta tatizo la kushindwa kupumua vizuri
  14. UTENDAJI KAZI WA MAPAFU
    Huboresha utendaji kazi wa mapafu na hivyo ni msaada mkubwa kwa wagonjwa wa pumu
  15. UGONJWA WA MTOTO WA JICHO (CATARACTS)Husaidia sana kupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa wa mtoto wa jicho (cataracts) yaani ukungu kwenye lenzi za macho; na hivyo huzuia macho kupoteza uwezo wa kuona
  16. KIFUA KIKUU
    Inaweza kusaidia katika matibabu ya kifua kikuu. Baadhi ya tafiti zimeonyesha kuwa vitamini C ina uwezo wa kuua bacteria wanaosababisha maradhi ya kifua kikuu.
    _______________________________________________________________________
X
2
Katika makala yetu iliyotangulia tulianza kwa kuwaeleza wasomaji wetu kuwa magonjwa yamegawanyika katika makundin mawili makuu, yaani magonjwa ya kimfumo na magonjwa ya kuambukiza. Tulitaja sababu kuu nne zinazozalisha magonjwa ya kimfumo, na kusema kuwa miongoni mwa sababu hizi ni ile inayohusu upungufu wa viini lishe fulani fulani ndani ya mwili ambavyo ni muhimu katika kuimarisha siha na kuendeleza uhai. Aidha tulisema kwamba kujitibu kwa chai ya Haiiba Timamu ni kwa kujirejeshea viini lishe mbalimbali ndani ya mwili, na tukasema kuwa tutazungumzia kupitia makala hizi makundi mbalimbali ya viini lishe vinavyopatikana katika chai hii, na faida za viini lishe hivi katika siha zetu. Tulimalizia makala yetu kwa kuzungumzia kundi la vitamini zinazopatikana ndani ya chai ya Haiiba Timamu na faida ya vitamini hizi katika siha. Makala ya pili katika mfululizo wa makala hizi itazungumzia kundi la pili la viini lishe vilivyomo ndani ya chai ya Haiiba Timamu. Kundi hili linahusisha madini lishe.

MADINI LISHE NI NINI?
Madini lishe ni viasili (elements) visivyo vya kiorganiki (havina kiasili cha carbon ndani yake) ambavyo hupatikana kwenye udongo na maji; na ambavyo vinatumiwa na mimea kama sehemu ya chakula chao. Wanadamu na wanyama hupata madini lishe yanayohitajika mwilini kwa kula mimea. Upungufu wa madini lishe mwilini hupelekea kuathirika kwa ile michakato ya kibailojia inayosukumwa na uwepo wa madini hayo na hivyo kuzaa ugonjwa au magonjwa yanayohusiana na upungufu huo.
Kwa kawaida huwa tunatakiwa tupate madini lishe yote tunayohitaji kupitia katika lishe. Hata hivyo kutokana na mapungufu mbalimbali yaliyoko katika lishe zetu inatokea tukawa na upungufu wa baadhi ya madini lishe na hivyo kukumbwa na magonjwa yanayohusiana na huo upungufu.
MADINI LISHE MUHIMU YALIYOKO KATIKA HAIIBA TIMAMU TEA
Baadhi ya madini lishe muhimu yaliyoko kwa wingi katika chai hii ni Kalisi (calcium), Shaba (copper), Chuma (Iron), Magnesium, Phosphorous, Potassium, Zinc, Chromium na Manganese.
Kalisi (Calcium)
Faida za Kalisi ni nyingi. Faida saba muhimu ni pamoja na:

  1. KUPUNGUZA UNENE
    Tafiti zinaonyesha kuwa ulaji wa vyakula vyenye kalisi kwa wingi huongeza kasi ya kuunguza mafuta ndani ya mwili
  2. KUPAMBANA NA SARATANI
    Tafiti zimeonyesha kuwa wingi wa kalisi na vitamini D kwenye chakula hupunguza uwezekano wa kupata saratani hasa za kwenye utumbo mkubwa
  3. KISUKARI CHA UKUBWANI
    Tafiti zinaonyesha kuwa wingi wa kalisi na vitamini D kwenye chakula hupunguza uwezekano wa kupata kisukari cha ukubwani, na hasa kwa wanawake
  4. UJAUZITO
    Tafiti zinaonyesha kuwa wingi wa kalisi na vitamini D kwenye chakula huimarisha mbegu za kiume na kuondoa vizuizi kwa mayai ya mwanamke kutunga mimba
  5. VUGUVUGU LA KABLA YA HEDHI
    Inasaidia kupambana na VUGUVUGU la kabla ya hedhi (Premenstrual syndrome). Hii ni hali inayowapata baadhi ya wanawake kiasi cha juma moja hivi kabla ya kupata hedhi. Dalili za hali hii ni pamoja na chunusi, matiti yaliyojaa na kuwa laini, uchovu, kukosa usingizi, tumbo kujaa gesi, kukosa choo au kuharisha, kuumwa na kichwa au mgongo, kukosa hamu ya kula, au kuvamiwa na uchu wa baadhi ya vyakula, maumivu ya viungo na misuli, kupungukiwa na kumbukumbu, kukereka bila sababu, na mfadhaiko. Hata hivyo dailili hizi zinaweza kutofautiana baina ya mwanamke mmoja na mwingine.

  6. MARADHI YA KINYWA
     
    Inalinda dhidi ya maradhi ya kinywa, hususan yale yanayoshambulia fizi
  7. MIFUPA IMARA
    Inasaidia kujenga mifupa imara na kukinga dhidi ya maradhi ya mifupa.
Shaba (Copper)
Faida za Shaba ni nyingi. Faida tano muhimu ni pamoja na:

  1. KINGA ZA MWILI
    Husaidia kuondoa upungufu wa chembechembe nyeupe za damu na hivyo huongeza uwezo wa mwili kupambana na maambukizi
  2. MIFUPA IMARA
    Huimarisha mshikamano wa madini yanayounda mifupa na hivyo kupunguza uwezekano wa mtu kupata ugonjwa wa mifupa dhaifu (osteoporosis)
  3. UTENDAJI KAZI WA MISHIPA YA FAHAMU
    Huboresha utendaji kazi wa mishipa ya fahamu
  4. KUDUMAA KATIKA UKUAJI
     
    Hiondoa uwezekano wa kudumaa katika kukua
  5. UDHIBITI WA RANGI YA NYWELE NA NGOZI
    Hupunguza uwezekano wa kuchujuka kwa rangi ya nywele na ngozi.
Chuma (Iron)
Faida za Chuma ni nyingi. Faida tano muhimu ni pamoja na:

  1. DAMU
    Ni muhimu sana katka uundaji wa chembechembe nyekundu za damu (Hemoglobin)
  2. USAFIRISHAJI WA GESI YA OKSIJENI MWILINI
    Hufanya kazi kama kibebaji cha gesi ya oxygen na husaidia kusafirisha oxygen kati ya seli moja ya mwili na nyingine
  3. UTENDAJI KAZI WA MISULI
    Chuma ni kiambata muhimu cha protini aina ya myglobin inayopatikana kwenye misuli. Protini hii huchukua oxygen kutoka katika hemoglobin na kuisambaza katika maeneo yote ya msuli. Kitendo hiki kinahitajika ili misuli iweze kukaza na kukunjuka
  4. AFYA YA UBONGO
    Husaidia afya ya ubongo. Ubongo unahitaji 20% ya oxygen yote iliyoko mwilini. Chuma husaidia damu kuweza kubeba kiasi kikubwa cha oxygen na kwa hivyo husaidia kutunza afya ya ubongo
  5. UPUNGUFU WA DAMU
    Husaidia dhidi ya upungufu wa damu (anemia) na magonjwa yanayohusishwa na upungufu wa damu kama uchovu, udhaifu wa mwili, maumivu ya kichwa, ongezeko la hisia kali dhidi ya baridi, na baadhi ya magonjwa ya figo.
Magnesium
Haya ni madini yenye faida nyingi sana muhimu kiafya. Madini haya yanahitajika ili kusukuma zaidi ya michakato 300 ya kibailojia na kikemia ndani ya mwili. Baadhi ya faida hizi ni pamoja na:

  1. UJENZI WA MIFUPA
    Pale yanapotumika pamoja na madini ya kalisi husaidia kujenga upya mifupa iliyodhoofika
  2. SHAMBULIO LA MOYO NA KIHARUSI
    Madini haya hupunguza hatari ya kukumbwa na ugonjwa wa shambulio la moyo na kiharusi
  3. SHINIKIZO LA DAMU
    Husaidia kuratibu shinikizo la damu mwilini
  4. KISUKARI CHA UKUBWANI
    Husaidia kuzuia kisukari cha ukubwani na katika matibabu ya kisukari hicho. Tafiti zinaonyesha kuwa magnesium husaidia katika uchakataji wa wanga na katika utendaji kazi wa homoni ya insulin kwa namna ambayo hufanya kiwango cha sukari kwenye damu kuwa ndani ya wigo unaokubalika
  5. MAUMIVU YA KICHWA, KUKOSA USINGIZI NA MFADHAIKO
    Magnesium husaidia katika kutibu maumivu endelevu ya kichwa (migraines), kukosa usingizi na mfadhaiko
  6. MARADHI MBALIMBALI YA AKILI
     
    Magnesium hutibu pia maradhi ya kiakili kama hofu isiyo na sababu, msongo, na wasiwasi.

Phosphorous
Haya ni madini yenye faida nyingi muhimu kiafya. Baadhi ya faida hizi ni pamoja na: 

  1. SIHA YA MIFUPA NA MENO
    Madini haya hufanya kazi pamoja na kalisi kuimarisha meno na mifupa. Kuoza kwa meno na magonjwa ya fizi ni miongoni mwa dalili kubwa za upungufu wa phosphorous
  2. USAGAJI WA CHAKULA TUMBONI
    Huongeza ubora wa usagaji chakula tumboni na wepesi wa kupata haja kubwa
  3. UCHOVU WA MWILI
    Husaidia kuondoa uchovu mwilini
  4. UZALISHAJ WA HOMONI
    Husaidia katika uratibu wa uzalishaji wa homoni, ikiwa ni pamoja na zile zinazohusiana na afya ya uzazi. Kupata kiasi cha kutosha cha phosphorous huongeza uwezekano wa kupata ujauzito na mimba kuwa salama
  5. UZALISHAJI WA PROTINI
    Phosphorous huhusika na mchakato wa kuzalisha protini ndani ya mwili. Protini ni muhimu katika kuhakikisha siha ya seli. Seli zinapoharibika huhitaji kujikarabati na kuunda seli nyingine. Uwepo wa phosphorous na protini huwezesha zoezi hili kufanyika kwa weledi
  6. SIHA YA UBONGO
    Phosphorous ni miongoni mwa viini lishe vinavyopatikana kwa wingi ndani ya seli za ubongo. Hii ina maana kuwa ili ubongo ufanye kazi vizuri mwili unahitaji kuwa na kiasi cha kutosha cha phosphorous.

Potassium
Haya ni madini yenye faida nyingi muhimu kiafya. Baadhi ya faida hizi ni pamoja na:

  1. MZUNGUKO WA DAMU
    Husaidia siha ya mfumo wa mzunguko wa damu na kuwezesha shinikizo sahihi la damu. Tafiti nyingi zimethibitisha kuwa kiwango kidogo cha madini ya potassium mwilini husababisha maradhi ya mfumo wa mzunguko wa damu na ongezeko la shinikizo la damu
  2. MIFUPA NA MISULI
     
    Potassium huongeza pH ya vimiminika vilivyoko mwilini (body fluids) na hivyo kusaidia kuzimua tindikali inayolundikana mwilini kutokana na lishe na sababu nyingine na hivyo kuzuia maradhi mbalimbali hasa yale ya mifupa na misuli
  3. SUKARI YA KUSHUKA
    Husaidia kuzuia kuporomoka kupita kiasi kwa kiwango cha sukari kwenye damu
  4. UTENDAJI KAZI WA MISULI
    Huhitajika katika mchakato wa kubana na kuachia kwa misuli. Kiasi cha kutosha cha potassium kinahitajika kwa ajili ya kazi hii. Kiasi cha potassium kinapokuwa kidogo kuliko inavyohitajika misuli itashindwa kufanya kazi zake ipasavyo na mtu atapata tatizo la kushikwa na misuli (muscle cramps).
  5. UTENDAJI KAZI WA UBONGO
    Potassium ina majukumu kadhaa yanayowezesha ubongo kufanya kazi kwa weledi. Majukumu haya ni pamoja na lile la kuusaidia ubongo kusafirisha umeme, kuboresha uhifadhi wa kumbukumbu na uwezo wa kujifunza. Imebainika pia kuwa upungufu wa potassium unaweza kusababisha maradhi ya akili kama vile kifafa.
  6. UVUNJIFU NA UJENZI WA KEMIKALI MWILINI (METABOLISM)
    Potassium husaidia katika kuchakata vyakula aina ya wanga na mafuta. Hii ina maana kuwa potassium ina umuhimu mkubwa katika kutoa nishati iliyoko ndani ya vyakula kutoka katika makundi haya pale tunapovila. Tafiti pia zimeonyesha kuwa potassium ina mchango kiasi fulani katika uundaji na ujenzi wa protini ndani ya mwili. Bila protini tishu za mwili hazitaweza kujiunda upya, seli hazitaweza kukua ipaswavyo na ujenzi na uvunjifu wa kemikali mwilini (metabolism) katika ujumla wake hautakwenda sawa
  7. MSONGO NA MFADHAIKO
    Potassium ina mchango mkubwa katika kudhibiti homoni zinazohusishwa na msongo na mfadhaiko. Homoni hizi zikiachiwa ziwepo kwa wingi mwilini bila kuratibiwa zinaweza kusababisha madhara makubwa ya kiafya ikiwa ni pamoja na kuporomoka kwa kinga za mwili
  8. MSAADA KWA FIGO
    Potassium husaidia figo kuondoa uchafu mwilini.
  9. UWIANO WA MAJI MWILINI (WATER BALANCE)
    Potassium husaidia seli za mwili kuhifadhi maji katika uwiano unaotakiwa.
  10. USAFIRISHAJI WA UMEME NDAN YA MWILI
    Potassium ni madini yenye uwezo wa kubeba umeme kwa ufanisi mkubwa (electrolyte). Electrolyte husafirisha umeme kati ya ubongo, mfumo wa neva na maeneo mengine ya mwili na kukifanya kila kiungo cha mwili kufanya kazi kwa weledi na kama ilivyokusudiwa
  11. MFUMO WA NEVA
     
    Potassium husaidia kuboresha utendaji wa mfumo wa neva unaosafirisha ujumbe baina ya sehemu moja ya mwili na nyingine.

Zinc
Haya ni madini yenye faida nyingi muhimu kiafya. Baadhi ya faida hizi ni pamoja na:

  1. SIHA YA NGOZI
    Zinc ina manufaa makubwa kama tiba dhidi ya chunusi na magonjwa mengine ya ngozi. Inaboresha utendaji wa seli nyeupe za damu kitendo ambacho husaidia sana katika  kupambana na maambukizi yakiwa ni pamoja na yale yanayoshambulia makovu, vidonda, vidonda vya moto na majeraha mengine. Zinc pia inahitajika katika uundaji wa collagen, protini ambayo inatumika kama malighafi muhimu katika uundaji wa tishu zinazotumika kama kiungo baina ya kiungo kimoja na kingine. Collagen huhitajika katika ukarabati wa ngozi na utengenezaji wa ngozi mpya
     
  2. UKURUTU (ECZEMA)
     
    Huzuia ugonjwa wa ukurutu (Eczema)
  3. HOMONI YA KIUME (TESTESTERONE)
    Huratibu na kudhibiti wingi wa homoni ya kiume (Testosterone) mwilini.
  4. TEZI DUME
    Hudhibiti matatizo ya tezi dume (prostate disorders). Upungufu wa zinc husababisha kuvimba kwa tezi dume, kitendo ambacho kinaweza kusababisha tezi hiyo kukumbwa na saratani
     
  5. UTENDAJI KAZI WA UBONGO
    Madini ya zinc yako kwa wingi katika eneo la ubongo linaliotwa hippocampus. Eneo hili huhusika na masula ya kufikiri na kumbukumbu. Kwa wale wenye matatizo ya ubongo yaliyotokana na majeraha, wingi wa zinc mwilini utasaidia kuufanya ubongo ufanye kazi vizuri kwa sababu moja ya kazi za zinc ni kutibu majeraha pia. Aidha tafiti zimeonyesha kuwa zinc inapoungana na vitamini B6 huboresha utendaji wa kemikali tarishi (neurotransmitters) zinazofanya kazi ya kusafirisha taarifa baina ya pande mbalimbali za mwili
  6. VIONJO VYA HARUFU
    Zinc pia huboresha utendaji kazi wa vionjo vya harufu na ladha. Tafiti zimeonyesha kuwa ongezeko la zinc humwilini huongeza ufanisi wa vionjo hivi kwa kiasi kikubwa
  7. UGONJWA WA MAFUA
    Zinc husaidia pia katika kupunguza makali ya ugonjwa wa mafua na kuufanya upone haraka. Hii inatokana na ukweli kwamba madini haya yanaboresha utendaji kazi wa chembechembe nyeupe za damu na hupunguza chembe za cytokines zinazochochea mfuro (inflammation) ambao kwa upande wake huongeza ukali wa mafua.


Chromium
Haya ni madini yenye faida nyingi muhimu kiafya. Baadhi ya faida hizi ni pamoja na:

  1. UCHAKATAJI WA WANGA, MAFUTA NA PROTINI
    Huratibu uchakataji wa wanga, mafuta na protini na kuongeza uwezo wa homoni ya insulin kufanya kazi yake na hivyo kusaidia katika kudhibiti kisukari cha ukubwani (type II diabetes).
  2. UCHU WA KULA MARA KWA MARA
     
    Husaidia kupunguza uchu wa kutaka kula mara kwa mara 
     
  3. KURATIBU LEHEMU (CHOLESTEROL)
    Husaidia kuratibu wingi wa lehemu (cholesterol) mwilini
  4. SHINIKIZO LA DAMU
    Hukinga dhidi ya ongezeko la shinikizo la damu.

Manganese
Haya ni madini yenye faida nyingi muhimu kiafya. Baadhi ya faida hizi ni pamoja na:

  1. MIFUPA IMARA
    Madini haya ni ya lazima katika ujenzi wa mifupa imara. Husaidia sana katika kuhifadhi na kulinda mifupa ya uti wa mgongo
  2. KIZUIA KIOKSIDISHAJI
    Madini haya hufanya kazi kama kizuia kioksidishaji chenye nguvu na hivyo kusaidia kulinda mwili dhidi ya chembe zilizobeba umeme chanya (free radicals) zinazozalishwa mwilini katika mchakato wa kawaida wa ujenzi na uvunjifu wa kemikali mwilini, na ambazo zina madhara makubwa kiafya
  3. KUSAWAZISHA SUKARI KWENYE DAMU
    Husaidia kuweka kiwango cha sukari katika damu kuwa katika hali ya kawaida. Ili kutekeleza jukumu hili madini haya huweka sawa uzalishaji wa homoni ya insulin ndani ya mwili na pia huzuia kuporomoka kusiko tabirika kwa sukari mwilini kwa wale ambao ni wagonjwa wa sukari
  4. KIFAFA
    Husaidia kuzuia shambulio la ugonjwa wa kifafa
  5. UTENDAJI KAZI WA VIMENG'ENYA
    Huamsha baadhi ya vimeng’enya ambavyo vina jukumu katika uchakataji wa lehemu (cholesterol), vijenzi vya protini (amino acids) na wanga. Aidha huhusika katika uchakataji wa viini lishe vya vitamini E na Vitamini B1 na pia hulisaidia ini kufanya kazi kwa weledi na ufanisi
  6. KUDHIBITI MFURO NA MITEGUKO
    Husaidia kudhibiti mfuro (inflammation) na miteguko. Inaaminika kwamba msaada huu hutokana na uwezo wa manganese kuongeza kemikali ya superoxide dismutase (SOD). Kemikali hii ina uwezo mkubwa wa kupambana na mfuro na hivyo ni msaada mkubwa sana kwa wagonjwa wa jongo na baridi ya abisi
  7. MATATIZO YA HEDHI
    Husaidia kukabiliana na matatizo yanayohusiana kukaribia kuingia kwenye hedhi (Pre-menstrual syndrome)
  8. UTENDAJI KAZI WA HOMONI YA THYROXINE
    Ni kiambata muhimu cha homoni ya thyroxine. Homoni hii ni muhimu sana katika kuendesha mchakato wa ujenzi  na uvunjifu wa kemikali ndani ya mwili (metabolism)
  9. MATUMIZI YA VITAMINI MWILINI
    Husaidia sana katika ufyonzwaji wa vitamini mwilini. Ufanisi wa ufyonzwaji wa vitamini muhimu mwilini kama vitamini E na vitamini B1 pamoja na madini ya magnesium hutegemea sana uwepo wa madini ya manganese
  10. UTENDAJI WA UBONGO
    Manganese ni muhimu kwa ajili ya utendaji bora wa ubongo na pia husaidia sana katika tiba ya matatizo yanayohusiana na mfumo wa neva. Inaaminika kuwa hii ni kutokana na manganese kuchochea kuzalishwa kwa superoxide dismutase (SOD). Kemikali hii hufanya kazi ya kusaka chembechembe zenye umeme chanya (free radicals) kila mahala mwilini na kuzizimua kabla hazijasababisha madhara makubwa ya kiafya
  11. UCHAKATAJI WA GLUCOSE
    Husaidia katika uchakataji wa glucose na kuifanya ifanye kazi barabara ndani ya mwili na kuzuia ongezeko la ziada ndani ya damu, kitu ambacho ni hatari kwa wagonjwa wa kisukari
  12. MFUMO WA USAGAJI CHAKULA
    Husaidia utendaji kazi wa mfumo wa usagaji chakula na hivyo kuboresha ufyonzwaji wa virutubisho na uondoshaji wa uchafu mwilini kwa njia ya haja kubwa.
_______________________________________________________________________________
                                                           
 3
Katika kujenga hoja ni kwa nini chai ya Haiiba Timamu inamfaa kila mtu, tumeshatoa makala mbili tayari. Hoja ya msingi iliyotawala makala zote mbili, na ambayo tunaiendeleza katika makala hii ni ile inayoelezea kuwa tiba ya chai hii inatokana na kumrejeshea mhusika viini lishe mbali mbali vilivyopungua mwilini mwake, ambavyo ni muhimu katika kujenga siha bora. 

Katika makala zilizotangulia tulizungumzia viini lishe vya vitamini na madini lishe vilivyomo ndani ya Haiiba Timamu Tea. Katika makala yetu ya pili tulizingimzia madini lishe yote yaliyoko katika chai ya Haiiba Timamu. Makala yetu ya leo itazungumzia kundi la tatu la viini lishe. Hili ni kundi la viini lishe vinavyojulikana kama vijenzi vya protini au tindikali za amino (amino acids).

TINDIKALI ZA AMINO AU VIJENZI VYA PROTINI
VIJENZI VYA PROTINI NI NINI?
Vijenzi vya protini ( tindikali za amino/amino acids) ni molekuli (molecule) ndogondogo zinazotumika kama tofali za kuundia protini. Protini ni molekuli (molecule) kubwa za kibaiolojia zenye majukumu kadhaa wa kadhaa ndani ya mwili. Idadi kubwa ya shughuli mbali mbali katika seli za mwili hufanywa na protini. Aidha protini zinahitajika katika uratibu na utendaji kazi wa tishu na viungo vya mwili, ikiwa ni pamoja na kuunda maumbo ya tishu na viungo husika. 
Protini huundwa na mamia au maelfu ya molekuli za tindikali za amino zilizoungana katika umbile la nyororo. Kuna tindikali za amino 20 zinazoweza kuungana katika michanganyiko mbalimbali (combination) kutengeneza molekuli za protini.  Kwa kawaida huwa tunatakiwa tupate vijenzi vyote vya protini tunavyohitaji kupitia katika lishe. Hata hivyo kutokana na mapungufu mbalimbali yaliyoko katika lishe zetu inatokea tukawa na upungufu wa baadhi ya hivi vijenzi vya protini na hivyo kukumbwa na magonjwa yanayohusiana na huo upungufu.
VIJENZI MUHIMU VYA PROTINI VILIVYOKO KATIKA HAIIBA TIMAMU TEA
Baadhi ya vijenzi muhimu vya protini vilivyoko kwa wingi katika chai hii ni Arginine, Histidine, Isoleicine, Leucine, Lysine, Methionine, Phenylalanine, Threonine, Tryptophan, na valine..
Arginine
Faida za argininei ni nyingi. Miongoni mwa faida hizi ni pamoja na:
  1. KUPONA MAJERAHA
    Huongeza kasi na ufanisi wa kupona majeraha
  2. UFANISI WA FIGO
    Huongeza ufanisi wa figo katika kuondosha uchafu mwilini
  3. KINGA ZA MWILI
    Huboresha kinga za mwili na utendaji kazi wa homoni
  4. MZUNGUKO WA DAMU
    Huboresha mzunguko wa damu na hivyo huusaidia moyo kufanya kazi kwa ufanisi kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa yanayohusiswa na mkakamo wa mishipa ya damu kama shinikizo la damu, kupoteza nguvu za kiume, shambulizi la moyo na maumvu ya kifua yanayosababishwa na mzunguko dhaifu wa damu (angina);
Histidine
Faida za Shaba ni nyingi. Miongoni mwa faida hizi ni pamoja na:

  1. HAMU YA TENDO LA NDOA
    Husaidia uongeza hamu ya tendo la ndoa
  2. KINGA ZA MWILI
    Inahusika katika uzalishaji wa chembe nyeupe na chembe nyekundu za damu. Ni kinga nzuri dhidi ya upungufu wa kinga mwilini, kinga  dhidi ya madhara ya mionzi hatari na pia husaidia kuondoa mlundikano wa madini mazito ndani ya mwili

Isoleucine
Faida za Isoleucine ni nyingi. Miongoni mwa faida hizi ni pamoja na:

  1. UZALISHAJI WA CHEMBECHEMBE NYEKUNDU ZA DAMU
    Kutengeneza chembechembe nyekundu za damu (Hemoglobin)

  2. UKARABATI WA TISHU
    Inachochea ukarabati wa tishu baada ya upasuaji au ajali
  3. MAGONJWA YA AKILI
    Inaleta unafuu kwa magonjwa mbalimbali ya akili kama msongo endelevu, mfadhaiko, kukosa usingizi, nakadhalika

  4. KUIMARISHA MISULI
    Inazuia misuli isiharibike wakati wa kufanya mazoezi
  5. NGUVU MWILINI
       Inaongeza nguvu mwilini

  6. KUHIMILI KAZI NGUMU
    Inajenga uwezo wa mwili kuhimili kazi ngumu

Leucine
Hii ni miongoni mwa tindikali za amino ambazo hazizalishwi ndani ya miili yetu na kwa hivyo ni lazima kuipata kupitia lishe. Faida za Leucine ni nyingi. Miongoni mwa faida hizi ni pamoja na:

  1. UIMARA WA MISULI
    Inachagiza ujenzi wa protini zinazounda misuli mbalimbali ya mwili
  2. KUDHIBITI UZITO WA MWILI
    Humsaidia mtu anayepunguza kula ili kupunguza uzito kuunguza mafuta yaliyolundikana mwilini, bila kuathiri misuli
  3. UJENZI WA MISULI MIPYA
    Inachagiza kemikali moja inayokaa kwenye misuli inayoitwa m-TOR (mammalian target of rapamycin) ambayo hufanya kazi kama ‘swichi’ ya kuwezesha uzalishaji wa protini zinazohitajika katika kujenga misuli kufanya kazi kikamilifu.
             
Lysine
Hii ni miongoni mwa tindikali za amino ambazo hazizalishwi ndani ya miili yetu na kwa hivyo ni lazima kuipata kupitia lishe. Faida za Lysine ni nyingi. Miongoni mwa faida hizi ni pamoja na:

  1. KIWANGO CHA LEHEMU (CHOLESTEROL)
    Husaidia kuratibu kiwango cha lehemu (cholesterol) mwilini
  2. SIHA YA MIFUPA Ni muhimu sana katika kulinda afya ya mifupa. Inasaidia mwili kupokea na kutumia madini ya kalisi (calsium) kwa weledi zaidi na pia husaidia kupunguza upoteaji wa kalisi kutoka katika mifupa
  3.  UDHIBITI WA VIRUSI AINA YA HERPES
    Huzuia kuzaliwa kwa virusi aina ya Herpes na husaidia kuongeza kasi ya kupona kwa watu waliopata maradhi yanayosababishwa na virusi hivyo
  4. MKANDA WA JESHI
    Husaidia kupunguza makali ya ugonjwa wa mkanda wa jeshi (shingles)
  5. MSONGO NA MFADHAIKO
    Humsaidia mtu kupungukiwa na matatizo ya msongo na mfadhaiko
  6.  MAUMIVU MWILINI
    Husaidia kupunguza maumivu ndani ya mwili
  7. MZUNGUO WA DAMU
    Husaidia kuboresha siha ya moyo na mfumo wa mzunguko wa damu kwa ujumla.
Methionine
Hii ni miongoni mwa tindikali za amino ambazo hazizalishwi ndani ya miili yetu na kwa hivyo ni lazima kuipata kupitia lishe. Faida za Lysine ni nyingi. Miongoni mwa faida hizi ni pamoja na:

  1. MAFUTA MWILINI
    Husaidia kuchakata na kuondoa mafuta mwilini
  2. UGONJWA WA INI BONGE
    Inazuia mlundikano wa mafuta kwenye ini na hivyo kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa ini bonge (fatty liver disease)
  3. UFANISI WA MISULI
    Inahitajika katika utengenezaji wa creatine. Creatine ni kiini lishe kinachohitajika katika uzalishaji wa nishati inayohitajika katika kuifanya misuli ifanye kazi zake kwa ufanisi
  4. UUNDAJI WA COLLAGEN Inahitajika katika uzalishaji wa protini aina ya collagen ambayo ni muhimu katika uundaji wa ngozi, kucha na tishu zinazounganisha misuli
  5. VIRUSI VYA UKIMWI
    Husaidia kuimarisha siha za watu wanaoishi na virusi vya ukimwi
  6. MFURO (INFLAMMATION) WA KONGOSHO (PANCTREATITIS)
     
    Husaidia kupunguza mfuro (inflammation) wa kongosho yaani pancreatitis
  7. UGONJWA WA PARKINSON
    Husaidia kupunguza dalili za ugonjwa wa Parkinson
  8. MAAMBUKIZI YA NJIA YA MKOJO
    Husaidia kukabiliana na maambukizi katika njia ya mkojo

 Phenylalanine
Faida za Lysine ni nyingi. Miongoni mwa faida hizi ni pamoja na:

  1. MFADHAIKO
    Husaidia kukabiliana na mfadhaiko
  2.  UTUKUTU
    Huleta utulivu kwa watu wanaokabiliwa na ugonjwa wa kukosa umakini na wenye kiwango kikubwa cha utukutu (Attention Deficit - Hyperactivity Disorder)
  3. UGONJWA WA PARKINSON
    Inapunguza dalili za ugonjwa wa Parkinson
  4.  MAUMIVU MWILINI
    Husaidia kukabiliana na maumivu ndani ya mwili
  5. BARIDI YA ABISI (ARTHRITIS)
    Husaidia kukabiliana na ugonjwa wa baridi ya yabisi
  6. KUCHUJUKA RANGI YA NGOZI (VITILIGO)
    Husaidia kukabiliana na ugonjwa wa vitiligo (ugonjwa wa kuchujuka rangi ya ngozi
            
Threonine
Hii ni miongoni mwa tindikali za amino ambazo hazizalishwi ndani ya miili yetu na kwa hivyo ni lazima kuipata kupitia lishe. Faida za Lysine ni nyingi. Miongoni mwa faida hizi ni pamoja na:

  1. UWIANO WA PROTINI NDANI YA MWILI
    Huratibu uwiano wa protini ndani ya mwili ili kudhibiti upungufu

  2. UJENZI WA PROTINI MWILINI
    Huratibu uwiano wa protini ndani ya mwili ili kudhibiti upungufu
  3. UTENGENEZAJI WA TINDIKALI ZA AMINO ZA GLYCNE NA SERINE
    Inatengeneza tindikali za amino za glycine na serine 2 ambazo ni muhimu sana katika uundaji wa protini aina za collagen na elastin ambazo ni vitu muhimu sana kwa siha ya ngozi, tishu zinazounganisha misuli na mishipa ya damu

  4. TABAKA LA NJE LA MENO MENO
    Inatengeneza tabaka jembamba linalozunguka jino kwa nje (tooth enamel)
  5. KUONDOA MAFUTA KWENYE INI
    Inashirikiana na methionine na tindikali aina ya aspartic (aspartic acid) kuliwezesha ini kuondokana na mafuta
  6. SUKARI KWENYE DAMU 
    Inafanya sukari ya damu isiongezeke au kupungua kiholela
  7. KINGA ZA MWILI
    Inaboresha mfumo wa kinga za mwili
  8. UKUAJI WA TEZI YA THYMUS
    Ina umuhimu wa kipekee katika ukuaji wa tezi ya thymus katika ubongo

  9. MFUMO WA MISHIPA YA FAHAMU
    Ni ya lazima kwa ajili ya siha bora ya mfumo wa mishipa ya fahamu

  10. MSONGO NA MFADHAIKO
    Inasaidia kupambana na msongo na mfadhaiko
  11. UZALISHAJI WA NISHATI KATIKA SELI ZA MWILI
    Inawezesha mchakato wa kikemia unaohitajika kuzalisha nishati katika seli (krebs cycle) kufanya kazi kwa ufanisi unaotakiwa
  12. MIFUPA IMARA 
    Husaidia ujenzi wa mifupa imara
  13. KASI YA KUPONA MAJERAHA
    Huongeza kasi ya kupona kwa majeraha

    ___________________________________________________________________________
                 
4
Makala hii ni ya nne na ya mwisho, kati ya mfulululizo wa makala zilizokusudiwa kujenga hoja juu ya chai ya Haiiba Timamu kuhitajiwa na kila mtu. Hoja ya msingi iliyotawala makala zote tatu zilizopita, na ambayo tunaiendeleza katika makala hii, ni kuwa tiba ya chai hii inatokana na kumrejeshea mhusika viini lishe mbali mbali muhimu vilivyopungua mwilini mwake. Katika makala zilizotangulia tulizungumzia makundi matatu ya viini lishe vilivyomo kwenye chai ya Haiiba Timamu. Tuliyataja makundi haya kuwa ni yale ya vitamini, madini lishe na tindikali za amino, au vijenzi vya protini. Makala hii ya mwisho itataja kundi la nne na la mwisho; hili si lingine bali ni kundi la vizuia vioksidishaji (anti-oxidants).

VIZUIA VIOKSIDISHAJI
VIZUIA VIOKSIDISHAJI NI NINI?
Vizuia vioksidishaji ni molekuli (molecule) zinazozuia mchakato wa kuoksidisha molekuli nyingine. Kuokisidisha ni muingiliano wa kikemia (chemical reaction) unaopelekea molekuli iliyookisidishwa kupoteza chembe yenye/zenye umeme hasi (electron), au kupoteza kiasili cha hydrogen katika umbile lake, au umbile lake kuongezewa kiasili cha oxygen.
Mchakato wa uoksidishaji ndani ya mwili hutokea muda wote. Huu ni sehemu ya mchakato wa ujenzi na uvunjifu wa kemikali ndani ya mwili, yaani metabolism. Mchakato wa kuoksidisha unaweza kuzaa chembechembe zenye umeme chanya zinazoitwa free radicals. Kwa upande wake hizi free radicals ni chembe zenye uwezo mkubwa wa kuoksidisha, na hivyo kuwepo kwake kunaweza kuzaa ‘gharika’ (chain reaction) ya uoksidishaji ndani ya seli za mwili. Hali hii inaweza kusababisha uharibifu mkubwa wa seli au hata kifo cha seli husika.
Vizuia vioksidishaji huzuia hizi gharika kutokea ndani ya seli. Badala yake hivi vioksidishaji huoksidisha hivi vizuia vioksidishaji na kwa hivyo kuacha seli za mwili zikiwa katika hali ya salama. Kwa kawaida mwili unamiliki na kuendeleza mifumo kadhaa ya vizuia vioksidishaji mbalimbali. Vizuia vioksidishaji hivi ni pamoja na glutathione, Vitamini C, Vitamini A, na Vitamini E; pamoja na vimeng’enya mbalimbali kama catalase, superoxide dismutase na peroxidases mbalimbali. Kuwepo kwa kiwango kidogo cha vizuia vioksidishaji au kuwepo kwa vimeng’enya ndani ya mwili vinavyozuia utendaji kazi wa hivi vioksidishaji, kunaweza kusababisha hali inayoiitwa ‘msongo wa uoksidishaji’ (oxidative stress), hali ambayo husababisha seli za mwili kuharibiwa na hata kufa. Tafiti zinaonyesha kuwa huu msongo wa uoksidishaji ni chanzo cha magonjwa mengi ya kimfumo ikiwa ni pamoja na saratani.

VIZUIA VIOKSIDISHAJI VILIVYOMO KATIKA HAIIBA TIMAMU TEA
Baadhi ya vizuia vioksidishaji muhimu vilivyoko kwa wingi katika chai hii ni Curcumin; Catechines, Flavonoids, Piperine, na Cinnamaldehyde.
Curcumin
Curcumin ni kemikali ya kiorganiki ambayo iko katika kundi pana la kemikali zinazojulikana kitaalamu kama polyphenols. Polyphenols ni kemikali za kiorganiki ambazo sehemu fulani katika maumbo yao kuna mkusanyiko wa viasili ulioko katika mpangilio maalum unaosababisha sehemu kubwa ya tabia za kikemia za kundi hilo unaoitwa ‘phenol’. Mkusanyiko wa aina hii katika kemikali za kiorganiki zinazounda kundi lolote huitwa FUNCTIONAL GROUP kwa lugha ya kikemia. FUNCTIONAL GROUP kwa tafsiri isiyo lazima ni MKUSANYIKO WA VIASILI ambavyo husababisha tabia ya kikemia ya kundi zima. Faida za curcumin ni nyingi. Miongoni mwa faida hizi ni pamoja na:

  1. KUTAKASA MAJERAHA
    Hutakasa majeraha dhidi ya bacteria na kuharakisha uponaji wake
  2. SARATANI
    Ina uwezo mkubwa wa kudhibiti ukuaji wa saratani ya mbalimbali na kuenea kutoka eneo moja la mwili hadi jingine
  3. SIHA YA INI
    Ni kitakasaji cha asili cha ini
  4. KUMBUKUMBU
    Inaweza kuzuia au kusimamisha kukua zaidi kwa ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer’s disease)
  5. MAUMIVU
    Ni kituliza maumivu cha asili
  6. KUPUNGUZA UNENE
    Inaratibu ujenzi na uvunjifu wa kemikali mwilini na kusaidia katika kuondoa unene
  7. MFADHAIKO
    Imekuwa ikitumika katika baadhi ya nchi, mathalani China, kama tiba ya mfadhaiko
  8. MAGONJWA YA BARIDI YA ABISI (ARTHIRITIS) NA JONGO (GOUT)
    Ni pozo dhidi ya maradhi ya baridi ya yabisi na jongo
  9. KUPONA MAJERAHA
    Inaharakisha kupona kwa majeraha na kuirejesha ngozi iliyoumizwa katika hali yake ya kawaida ndani ya muda mfupi
  10. UGONJWA WA PSORIASIS
    Inasaidia katika matibabu ya ugonjwa wa psoriasis (ugonjwa unaosababishwa na kukua kwa kasi kwa baadhi ya seli za ngozi kupelekea ngozi kuwa na mabaka ya rangi tofauti tofauti), pamoja na magonjwa mengine ya ngozi yanayotokana na mfuro (inflammation) wa seli za ngozi.
CatechinsHuu ni mkusanyiko wa vizuia vioksidishaji ambavyo kutokana na maumbo yao kufanana kwa karibu na tabia zao za kikemia kufanana pia, vimewekwa katika kundi moja la kemikali za kiorganiki. Hata hivyo kama ilivyo kwa curcumin ambayo tumetangulia kuitaja, catechins ni sehemu ya kundi kubwa zaidi la kemikali za korganiki zinazojulikana kama polyphenols.  Faida za catechins ni nyingi. Miongoni mwa faida hizi ni pamoja na:

  1. KULUNDIKANA KWA MAFUTA MWILINI Huhusishwa na kusaidia sana kuzuia mlundikano wa mafuta mwilini
  2. LEHEMU (CHOLESTEROL)
    Hushusha kiwango cha lehemu katika damu
  3. SHINIKIZO LA DAMU NA SUKARI
    Huzuia ongezeko la shinikizo la damu na sukari kwenye damu
  4. UGONJWA WA MAFUA
    Husaidia kuzuia kupatwa na ugonjwa wa mafua
  5. MAGONJWA YA KUAMBUKIZA
    Hupambana dhidi ya maambukizi ya bacteria
  6. HARUFU MBAYA KWENYE KINYWA
    Huzuia harufu mbaya kutoka katika kinywa
              
Flavonids
Flavonoids ni mkusanyiko mwingine wa vizuia vioksidishaji ambavyo kutokana na maumbo yao kufanana kwa karibu na tabia zao za kikemia kufanana pia, vimewekwa katika kundi moja la kemikali za kiorganiki. Kama ilivyo kwa curcumin na catechins, vizuia vioksidishaji hivi pia viko katika kundi pana zaidi la kemikali za kiorganiki za polyphenols. Faida za flavonoids ni nyingi. Miongoni mwa faida hizi ni pamoja na:

  1. KUPAMBANA NA SARATANI Inaaminika kuwa zina uwezo mkubwa sana wa kupambana na saratani
  2. MAGONJWA YA MOYO
    Inaaminika kuwa zina uwezo mkubwa sana katika kukabiliana na magonjwa mbalimbali yanayohusiana na moyo
  3. MFURO (INFLAMMATION) Inaaminika kuwa zina uwezo mkubwa sana wa kukabiliana na mfuro wa seli.
Piperine
Piperine ni miongoni mwa kemikali za kiorganiki zinazoitwa alkaloids. Alkaloid ni kemikali yoyote ya kiorganiki ambayo umbile lake linajumuisha ‘nyongo’ (base) yenye kiasili cha nitrogen. Faida za piperine ni nyingi. Miongoni mwa faida hizi ni pamoja na:
  1. UFYONZAJI WA VIINI LISHE VILIVYOMO KWENYE CHAKULA
    Husaidia kuongeza uwezo wa mwili kwa kiasi kikubwa wa kufyonza na kutumia viini lishe mbalimbali vinavyopatikana kwenye vyakula
  2. KUDHIBITI UZITO WA MWILI 
    Inaaminika kuwa inachochea ongezeko la kasi ya ujenzi na uvunjifu wa kemikali ndani ya mwili (accelerates metabolism) na hivyo kusaidia katika harakati za kudhibiti uzito wa mwili
  3. MFURO (INFAMMATION) WA SELI
    Inasaidia kudhibiti mfuro (inflammation) wa seli
  4. SARATANI  Inapunguza kasi ya ukuaji wa seli za saratani, hususan zile zinazohusiana na saratani ya mapafu
  5. MSONGO NA MFADHAIKO
    Inachagiza mwili kuzalisha homoni ya serotonin ambayo husaidia sana kujenga hali ya kujisikia furaha na hivyo ni nzuri katika kukabiliana na msongo na mfadhaiko
              
Cinnamaldehyde
Cinnamaldehyde ni miongoni mwa kemikali za kiorganiki zinazoitwa cinnemaldehydes.  cinnemaldehydes ni kemikali za kiorganiki ambazo hutoa harufu (mara nyingi ya kupendeza) na ambazo FUNCTIONAL GROUP yake ni ile inayokusanya viasili katika mpangilio unaojulikana kama ALDEHYDE. Cinnamaldehyde ni kemikali ya kiorganiki ambayo ina faida kubwa mwilini.
  1. KULAINISHA DAMU
    Inafanya kazi kwa kuzuia kuganda kwa damu kunakoweza kupelekea damu isitembee mwilini inavyopasa
  2.  MFURO (INFAMMATION)
    Inasaidia sana kupambana na mfuro wa seli na kwa hivyo husaidia sana katika magonjwa yote yanayosababishwa na mfuro
  3. MLUNDIKANO WA MAFUTA KWENYE INI Inazuia mlundikano wa mafuta kwenye ini na hivyo kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa ini bonge (fatty liver disease)
  4. UZALISHAJI WA CREATINE NDANI YA MWILI
    Inahitajika katika utengenezaji wa creatine. Creatine ni kiini lishe kinachohitajika katika uzalishaji wa nishati inayohitajika katika kuifanya misuli ifanye kazi zake kwa ufanisi
  5. UZALISHAJI WA COLLAGEN NDANI YA MWILI
    Inahitajika katika uzalishaji wa protini aina ya collagen ambayo ni muhimu katika uundaji wa ngozi, kucha na tishu za viungo vinavyofanya kazi ya kuunganisha viungo mbalimbali vya mwili
  6. KINGA ZA MWILI
    Husaidia kuimarisha siha za watu wanaoishi na virusi vya ukimwi
  7. MFURO WA KONGOSHO (PANCREATITIS) 
    Husaidia kupunguza mfuro (inflammation) wa kongosho yaani pancreatitis
  8. UGONJWA WA PARKINSON
    Husaidia kupunguza dalili za ugonjwa wa Parkinson
  9. MAAMBUKIZI KATIKA NJIA YA MKOJO 
    Husaidia kukabiliana na maambukizi katika njia ya mkojo
          


X
X
X
X
X
X
X
X
X
X
X
X
X
X
X
X
X
X
X
X
X
X

2 comments:

  1. asante! je Hiyo TIMAMU TEA , mtu anayenyonyesha mtoto mchanga kabisa anaruhusiwa kuitumia?

    ReplyDelete
  2. niligunduliwa na saratani mnamo 2019 na nimekuwa nikitafuta tiba tangu wakati huo. Oktoba mwaka jana nilipokaribia kukata tamaa, nilikutana na chapisho kwenye mtandao ambapo nilinakili barua pepe ya mwanamume anayeitwa dr DAWN inayotoa suluhisho la mitishamba kwa magonjwa. niliwasiliana naye na kupata maelewano naye akanitumia dawa ya mitishamba kupitia united parcel service pamoja na maelekezo ya jinsi ya kuitumia. kwa mshangao wangu mkubwa, nilipona baada ya siku 14 za kutumia dawa kama alivyohakikishiwa na daktari.
    Niliamua kushiriki hii kwa sababu najua kuwa kuna watu wengi huko ambao wanahitaji msaada. au umtumie ujumbe kwa WhatsApp.+2349046229159 Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com

    Anaweza pia kuponya magonjwa mengi kama hayo

    {1}VVU na UKIMWI

    {2}Kisukari

    {3}Kifafa

    {4} Saratani ya Damu

    {5} HPV

    {6} ALS

    ReplyDelete